Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Taaluma ya Wanyamapori Pasiansi

Hadithi
Wahifadhi wa Wanyamapori walipwe vyema

Shirika la ulinzi wa wanyama duniani WWF linataka walinzi wa wanyama pori katika mbuga za taifa kwenye mataifa ya Afrika walipwe fedha maalum kwa kuwakamata majangili.

Serikali  ya  Ujerumani  inatoa  fedha  kwa  ajili  ya  eneo  la  bonde  la mto  Kongo  na  kuwezesha  kile  kinachoitwa  malipo  ya  kazi kwa walinzi wa mbuga  ya  wanyama  ya  Salonga , ambao  pia  wanapatiwa fedha  hizo maalum. Immo Fischer , msemaji  wa  WWF  nchini Ujerumani  akijibu  swali  la  DW amesema:

"Fedha za kuwalipa walinzi  wa  mbuga  za  wanyama , ni jambo  la kawaida  na  linatumika  katika  nchi  nyingi  za  Afrika. Walinzi  wa mbuga za wanyama wanafanya  kazi za hatari  sana, na  muhimu sana, na kutokana  na  kazi  hizo  muhimu matokeo  yake  ni  malipo."

Mtu anapaswa  kutambua  kuwa , wazo  hili  limetokana  na  haja  ya kupunguza rushwa. Wakati mlinzi wa  mbunga  ya  wanyama akimkamata jangili na  jangili  huyo ana pembe  mbili  kwa  mfano  za tembo, malipo yake  ya mwaka yataongezeka haraka. Kwa malipo  haya kwa walinzi wa mbuga za  taifa tunataka  kuepuka, kuachiliwa  huru kwa majangili kwa  kuwapa rushwa walinzi.

 

Mhariri: Grace Patricia Kabogo