Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Taaluma ya Wanyamapori Pasiansi

Historia ya Taasisi

Taasisi ya Taaluma ya Wanyamapori Pasiansi (PWTI) ipo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii. Taasisi hii inapatikana katika Kata ya Pasiansi, Wilaya Ilemela, Mkoa wa Mwanza barabara ya Makongoro. Taasisi ina ukubwa wa eneo la ekari 10.6. Kwa upande wa magharibi Taasisi inapakana na mwambao wa Ziwa Victoria pamoja na ofisi za Kikosi Dhidi ya Ujangili na Ofisi za Malihai klabu kanda ya ziwa takribani kilometa 5 kutoka Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Saanane.

Taasisi ya Taaluma ya Wanyamapori Pasiansi (PWTI) ilianzishwa rasmi kwa tamko la serikali la mwaka 2020 namba 465 baada ya kuwepo tangu kuanzishwa kwake mwaka 1966 kwa Sheria ya Uhifadhi Wanyamapori Na. 5 ya mwaka 2009 (Wildlife Conservation Act (WCA) No. 5 of 2009). Kwa wakati huo Sheria ya Wanyamapori ilikuwa inajulikana kama ‘Fauna Conservation Ordinance’ of 1959 ambayo ilibadilishwa na kuwa Sheria ya kuhifadhi Wanyamapori Na. 12 ya Mwaka 1974 na hatimaye kubadilishwa kuwa WCA No. 5 of 2009.

Chuo hiki  kilipoanzishwa kilijulikana kama kituo cha kutoa mafunzo kwa Askari wa Maliasili ambapo kilijulikana kama ‘Natural Resource Institute’ (NRI) na 1970 kozi hiyo ilibadilishwa na kutoa mafunzo kwa Askari wa ulinzi wa Wanyamapori (Game Scout Training Centre).  Mafunzo yalitolewa kwa kufuata mfumo wa Jeshi usu (paramilitary). Majukumu makuu ya askari wahifadhi wanyamapori ilikuwa ni ulinzi wa mali na maisha ya wanadamu dhidi ya wanyamapori wakali na waharibifu (Problem animal control). Hii ni kwa sababu  kwa wakati huo idadi ya binadamu ilikuwa ni ndogo chini ya milioni tisa wakati idadi ya wanayamapori ilikuwa ni kubwa sana ikilinganishwa na hali ilivyo sasa. Mafunzo kwa askari yalitolewa ya muda wa miezi sita.  Aidha, kwa kadri idadi ya binadamu ilipoongezeka na hali ya matumizi ya wanyamapori kuongeza na hatimaye kuwepo kwa vitendo vya ujangili wa wanyamapori na biashara haramu ya kimataifa ya nyara za serikali Chuo hiki kilibadili mitaala na muda wa mafunzo ulibadilika kutoka miezi sita kuwa miezi tisa.

Tangu mwaka 1966 hadi 2000, Chuo hiki kilikuwa kikidahili wanachuo waliajriwa na sekta ndogo ya wanyamapori nchini. Hata hivyo, kutokana na Sera ya Taifa ya Uhifadhi Wanyamapori ya Mwaka 1998 iliyopitiwa upya mwaka 2007 ilionyesha umuhimu wa ushirikishwaji wa wadau mbalimbali katika uhifadhi wanyamapori; na mabadiliko ya Kanuni za Ajira kwa Utumishi wa Umma; PWTI ilianza kudahili wanachuo ambao hawana ajira. 

Kutokana na maelezo hayo tangu kuanzishwa mwaka 1966 hadi 2019 Chuo hiki kimepitia mitaala yake mara sita kama ifuatavyo;

  1. Miaka ya 1970 Chuo kilifanya mmabadiliko ya mitaala kutoka mtaala mpana wa mafunzo kwa askari wa maliasili (NRI) na kuwa kwa Askari Wahifadhi Wanyamapori (Game Scout Training Centre- GSTC).  Sifa za kujiunga na Chuo ilikuwa na waliohitimu darasa la saba na muda wa mafunzo ilikuwa miezi sita. Lugha ya kufundishia ilikuwa Kiswahili.
  2. Miaka 1980s kutokana na kuongezeka kwa vitendo vya ujangili hasa wa tembo na faru, mitaala ilipitiwa upya, na kuongeza zaidi mafunzo ya himasheria. Muda wa mafunzo uliongezwa kutoka miezi sita kuwa tisa. Jina la Chuo lilibadilika kutoka GSTC kuwa Pasiansi Wildlife Training Institute (PWTI).
  3. Miaka ya 1990s kutokana na mabadiliko ya Sera na Kanuni ya Ajira kwa Utumishi wa Umma, kuwa kiwango cha chini cha elimu kuajiriwa itakuwa kidato cha nne (Form four) na uwepo wa Sera ya Uhifadhi Wanyamapori ya Mwaka 1998 (2007) kulisababisha mitaala ya Chuo  kupitiwa upya na kusababisha mabadiliko ya sifa za kujiunga na Chuo, sifa za walimu wanaofundisha na lugha ya kufundishia ikwa kiingereza (English)
  4. Miaka ya 2000s (2002 na 2007)- Chuo kilisajiliwa na Baraza la Taifa la Ushauri wa Vyuo vya Ufundi (National Council for Technical Education- NACTE) mwaka 2002 na kupata idhibati ya kudumu mwaka 2007. Hivyo, chou kilisajiliwa kutoa kozi za ngazi ya cheti mbili ambazo ‘National Technical Award (NTA) level 4 and 5 (Basic and Technician Certificate in Wildlife Management).
  5. Mwaka 2014 Chuo kiliandaa Mpango Mkakati wa kwanza wa kuanzia Julai 2014- Juni 2019 ambao ulionyesha kuwa Dira ya Chuo ni kuwa kituo mahiri cha mafunzo ya Himasheria ya Wanyamapori (To be a center of Excellence in provide training in Wildlife Law Enforcement). Aidha, hali ya ujangili inchini ilikuwa mbaya hasa ujangili wa tembo na biashara haramu ya nyamapori. Hivyo, Chuo kilipitia upya mitaala yake ambapo mtaala uliweka mkazo kwenye masomo kuhusu Himasheria na Ulinzi wa Wanyamapori. Hivyo, jina la kozi zitolewazo zilibadilika  kuwa ‘Basic and Technician Certificate in Wildlife Management and Law Enforcement”
  6. Mwaka 2019; Chuo kimeandaa Mpango Mkakati wa II wa kuanzia Julai 2019 -Juni 2024. Mpango Mkakati huo, unaeleza Chuo kuongeza kozi nyingine kuhusu masuala ya waongoza wataali na usalaama wao (Tour guiding and Safety).  Hivyo, kwa kuzingatia sera, sheria na kanuni za kupitia mitaala na kwa kushirikiana na wadau wa uhifadhi wanyamapori nchini, Chuo kimepitia mitalaa inayotumika sasa za kozi ya BTCWLE na TCWLE na kuandaa mitaala mipya ya kozi za waongoza watalii kwa ngazi ya NTA level 4 and 5. Kozi hizi zimeanza kutolewa mwaka wa masomo 2020/2021

 Pamoja na maelezo hayo, Chuo hutoa mafunzo ya muda mfupi kulingana na mahitaji ya mteja. Kwa sasa tuna mitaala ya mafunzo ya muda wa kuanzia wiki mbili hadi miezi sita. Mafunzo hayo ni pamoja na ; matumizi ya TEHAMA katika ukusanyanji wa taarifa za uhifadhi wanyamapori, uchunguzi wa makosa ya wanayamapori, namna ya utunzaji wa vielelezo vya kesi za wanyamapori, udhibiti wa wanayamapori wakali na waharibifu, kuongoza watalii na kutoa tafsiri za maliasili (Interpretation in Wildlife Resources).