Core Value
Maadili ya Msingi
Uadilifu na Uwajibikaji: Tunakuhakikishia kiwango cha juu cha uadilifu katika utoaji wa huduma za utawala na uwajibikaji katika kutoa ujuzi na maarifa na tunaahidi kudumisha na kutoa taarifa sahihi.
Uwezo: Tunawahudumia wanafunzi waliodahiliwa kwa gharama nafuu bila kuhatarisha gharama za uendeshaji.
Hali ya kifedha: Tunajitahidi kuwa na mikakati thabiti inayotuhakikishia uwezo wa rasilimali fedha za kutosha.
Usikivu: Tunajitahidi kujibu mahitaji ya wateja kulingana na mabadiliko ya nyakati katika dunia.
Umahiri wa Watumishi: Tunajitahidi kukuza watumishi thabiti wenye sifa nzuri na wenye motisha ambao wanatekeleza dira na dhima ya Taasisi kwa viwango vinavyokidhi vigezo.
Tutahakikisha uhifadhi endelevu wa wanyamapori: Tunajitolea kwa uhifadhi endelevu wa wanyamapori.
Ubunifu Shirikishi: Tunajitahidi kujenga mahusiano mazuri na jamii.