Astashahada ya Awali ya Uongozaji Watalii na Usalama
Kozi ya Astashahada ya Awali ya Uongozaji Watalii na Usalama, imeandaliwa kwa ajili ya kuwaandaa vijana waliohitimu kidato cha nne kuwa Waongoza Watalii wenye Kuzingatia mbinu za Usalama katika shughuli zao za kila siku katika Taasisi za Serikali, Mashirika binafsi, Jumuiya za Hifadhi za Vijiji, Makampuni ya Utalii, Uhifadhi na Uwindaji na Mashirika ya Kimataifa. Mafunzo haya yanatolewa kwa kipindi cha mwaka mmoja na yatamuwezesha mhitimu kufanya kazi za kawaida za kila siku katika Taasisi, Kampuni na Mashirika tajwa. Kazi hizo ni kama ifuatavyo:
- Kuongoza Watalii katika vivutio vya aina mbalimbali Tanzania,
- Kuelezea tafsiri ya vivutio kwa lugha za Kiswahili na kimataifa,
- Kuwapa taarifa sahihi watalii katika kivutio husika,
- Kukusanya na kuweka takwimu za watalii na safari za kitalii,
- Kujibu malalamiko kutoka kwa Watalii,
- Kusimamia miundo mbinu ya eneo la utalii,
- Kutoa ushauri wa kitaalamu kwa Taasisi, Shirika na Kampuni iliyomwajiri,
- Kutunza kumbukumbu za vitabu/majalada/majarida ya kitalii,
- kufanya kazi za ulinzi na doria katika maeneo ya ndani na nje ya eneo la kazi,
kufanya shughuli zingine za kawaida zitakazotolewa na viongozi sehemu za kazi.
Code |
Module Title |
Mhula |
|
1 |
2 |
||
TMT 04101 |
Kanuni za Utalii |
√ |
|
TMT 04202 |
Kanuni za Huduma kwa Wateja |
|
√ |
TMT 04103 |
Misingi ya Ujuzi wa Kuongoza Watalii |
√ |
|
TMT 04104 |
Tafsiri ya Vivutio vya Utalii vya Kibaiolojia |
√ |
|
TMT 04205 |
Tafsiri ya Vivutio vya Utalii vya Kiutamaduni |
|
√ |
TMT 04206 |
Misingi ya Sheria za Utalii na Uhifadhi wa Maliasili |
|
√ |
TMT 04207 |
Misingi ya Usalama na Utalii |
|
√ |
TMT 04108 |
Huduma ya Kwanza na Matibabu ya Dharura |
√ |
|
TMT 04209 |
Kanuni za Ujasiliamali wa Biashara ya Utalii |
|
√ |
TMT 04110 |
Ujuzi wa Fani ya Mawasiliano |
√ |
|
TMT 04211 |
Mafunzo ya Awali ya Kompyuta |
|
√ |
TMT 04112 |
Ujuzi wa Mbinu za Maisha |
√ |
|
TMT 04213 |
Misingi ya Utengenezaji Magari |
|
√ |
FAIDA ZA KUSOMA KOZI YA MSINGI YA UFUNDI WA UONGOZAJI WATALII NA USALAMA
- Atafahamu kanuni za Uongozaji Utalii - Basics of Tour Guiding Skills
- Ataweza kutoa huduma kwa mteja kitaalamu - Customer Care Skills
- Ataweza kutafsiri vivutio vya kibailojia na kitamaduni kwa Ufasaha – Biological and Cultural Interpretation Skills
- Atafahamu Sheria za Utalii na Uhifadhi – Tourism and Conservation Laws
- Atafahamu Misingi ya Usalama na kutoa huduma ya Kwanza kwa Watalii – Tourism Safety, First aid and Emergency Care Skills
- Atapata Ujuzi wa Kutumia Tarakilishi – Computer Skills
- Atajifunza Ufundi wa Magari – Basics of Motor Vehicle Maintanance
NYOTE MNAKARIBISHWA