Astashahada ya Usimamizi wa Uongozaji Watalii na Usalama
Kozi ya Astashahada ya Usimamizi wa Uongozaji Watalii na Usalama ni ya mwaka mmoja na imeandaliwa kwa ajili ya wahitimu wa Kozi ya Astashahada ya Awali ya Uongozaji Watalii na Usalama, na vijana waliohitimu kidato cha sita. Wahitimu wanaandaliwa kuwa viongozi wa shughuli za Uongozaji Watalii na Usalama wakati wa kutekeleza majukumu katika Taasisi za Serikali, Mashirika binafsi, Jumuiya za Hifadhi za Vijiji, Makampuni ya Utalii, Uhifadhi na Uwindaji na Mashirika ya Kimataifa. Mafunzo haya yanatolewa kwa kipindi cha mwaka mmoja na yatamuwezesha mhitimu kufanya kazi za kawaida za kila siku katika Taasisi, Kampuni na Mashirika tajwa. Kazi hizo ni kama ifuatavyo:
- Kuratibu kazi za uongozaji Watalii katika vivutio vya aina mbalimbali Tanzania,
- Kufanya ubunifu wa kuboresha taarifa za vivutio katika eneo la kazi,
- Kuibua vivutio vipya na kuweka taarifa sahihi,
- Kuhakikisha taarifa za vivutio zinatolewa kwa lugha sahihi kwa Watalii,
- Kuhakikisha takwimu za watalii na safari za kitalii zimerekodiwa na kutunzwa ipasavyo,
- Kuhakikisha malalamiko kutoka kwa Watalii yamepatiwa suluhu stahiki,
- Kuhakikisha miundo mbinu ya eneo la utalii ni salama muda wote,
- Kutoa ushauri wa kitaalamu kwa Taasisi, Shirika na Kampuni iliyomwajiri,
- Kuhakikisha kuwa kumbukumbu za vitabu/majalada/majarida ya kitalii yanatunzwa ipasavyo,
- Kuratibu na kusimamia kazi za ulinzi na doria katika maeneo ya ndani na nje ya eneo lake la kazi,
- kufanya shughuli zingine za kawaida zitakazotolewa na viongozi sehemu za kazi.
Code |
Module Title |
Muhula |
|
1 |
2 |
||
TMT 05101 |
Kanunu za Utalii |
√ |
|
TMT 05102 |
Kanuni za Huduma kwa Wateja |
√ |
|
TMT 05103 |
Misingi ya Ukarimu |
√ |
|
TMT 05204 |
Uongozi wa Watalii na Mbinu za Tafsiri ya Vivutio vya Utalii |
|
√ |
TMT 05105 |
Tafsiri ya Wanyamapori na Mimea |
√ |
|
TMT 05206 |
Sheria za Utalii na Uhifadhi Maliasili |
|
√ |
TMT 05107 |
Mafunzo ya Ukakamavu na Ujuzi wa Silaha |
√ |
|
TMT 05208 |
Utalii na Mbinu za Usalama Porini |
|
√ |
TMT 05209 |
Tafsiri ya vivutio vya Kitamaduni na Kijiografia |
|
√ |
TMT 05210 |
Misingi ya Ikolojia |
|
√ |
TMT 05211 |
Ujasiliamali na Masoko katika Utalii |
|
√ |
TMT 05212 |
Kanuni Mtambuka za Utalii |
|
√ |
TMT 05213 |
Mafunzo ya Awali ya Udereva |
|
√ |
TMT 05114 |
Lugha za Kigeni |
√ |
|
TMT 05115 |
Mafunzo ya Kompyuta |
√ |
|