Habari
TANGAZO LA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA TAASISI YA TAALUMA YA WANYAMAPORI PASIANSI KWA MWAKA WA MASOMO 2026/2027
TANGAZO LA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA TAASISI YA TAALUMA YA WANYAMAPORI PASIANSI KWA MWAKA WA MASOMO
i. Mkuu wa Taasisi ya Taaluma ya Wanyamapori Pasiansi, Mwanza anapenda kuwajulisha wafuatao kuwa wamechaguliwa kujiunga na kozi ya Astashahada ya Awali ya Usimamizi wa Wanyamapori na Himasheria (BTCWLE), Astashahada ya Usimamizi wa Wanyamapori na Himasheria (TCWLE), Stashahada ya Usimamizi wa Wanyamapori na Himasheria (ODWLE), na Astashahada ya Awali ya Uongozaji Watalii na Usalama (BTCTGTS) kwa mwaka wa masomo 2026/2027.
ii. Uchaguzi huu umejumuisha pia maombi ya mwezi Machi 2026 ambayo yalitumwa kwa njia ya mtandao na njia ya kujaza fomu.
iii. Waliochaguliwa wanatakiwa kuripoti chuoni kuanzia tarehe 11 Oktoba hadi 18 Oktoba 2026 kwa ajili ya kuanza mafunzo. Fomu ya kujiunga inapatikana kupitia tovuti ya Taasisi www.pasiansiwildlife.ac.tz au kufanya mawasiliano yaliyopo mwisho wa tangazo hili.
iv. Ili kuthibitisha udahili wako unatakiwa ulipe TZS 1,000,000/= ikiwa ni sehemu ya ada ya mwaka mzima, kupitia ‘Control number’ utakayopewa na Taasisi. Malipo hayo yawe yamefanyika kabla ya tarehe 10 Septemba 2026. IKIWA HAUTALIPIA HADI TAREHE HII NAFASI YAKO ITATOLEWA KWA MUOMBAJI ANAYEFUATA NA NAFASI ITAKUWA IMEPOTEA.
BONYEZA HAPA KUPATA TANGAZO LA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA TAASISI KWA MWAKA 2026/2027
BONYEZA HAPATA KUPA FOMU YA KUJIUNGA NA KOZI YA DIPLOMA YA UHIFADHI WANYAMAPORI 2026
BONYEZA HAPA KUPATA FOMU YA KUJIUNGA NA KOZI YA ASTASHAHADA YA UHIFADHI WANYAMAPORI (TCWLE) 2026
BONYEZA HAPA KUPATA BEI YA VIFAA VINAVYOHITAJIKA KWA WANACHUO KATIKA DUKA LA TAASISI 2026
Imetolewa na;
Mkuu wa Taasisi
28 Agosti 2026