Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Taaluma ya Wanyamapori Pasiansi

Matukio
MAHAFALI YA KOZI FUPI YA ASKARI WA VIJIJI (VGS) KUTOKA MIKOA YA KIGOMA NA KATAVI TAREHE 4 JUNI 2022
  • 04th Jun, 2022
  • Pasiansi
  • 08:00AM-02:00PM

Mafunzo ya askari wa vijiji toka katika Mikoa ya Katavi na Kigoma waliokuwa jumla ya 87, ambapo wakiume ni 78 na wakike ni 9. Askari hawa wamegawanyika katika taasisi mbili ambazo ni TUUNGANE na JGI. TUUNGANE ina jumla ya askari 44, wakiume ni 37, wakike ni 7 na JGI ina jumla ya askari 43 wakiume ni 41 na wakike ni 2.

Mafunzo walioyapata ni pamoja na mbinu za udhibiti wa majangili,matumizi sahihi ya silaha, namna ya ukamataji wa jangili,sheria za uhifadhi wa maliasili, utimamu wa mwili, namna ya uogeleaji na uokoaji ndani ya maji,uteguaji wa mitego iliyotegwa na majangili, utoaji wa huduma ya kwanza na utumiaji wa vifaa vya TEHAMA kwenye uhifadhi wa maliasili.