Habari
TANGAZO LA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA TAASISI MACHI 2024
Mkuu wa Taasisi ya Taaluma ya Wanyamapori Pasiansi, Mwanza anapenda kuwajulisha wafuatao kuwa wamechaguliwa kujiunga na kozi ya Astashahada ya Awali ya Usimamizi wa Wanyamapori na Hima Sheria (BTCWLE) katika udahili wa Machi 2024 kwa mwaka wa masomo 2024/2025. Waliochaguliwa wanatakiwa kuripoti Jumatatu tarehe 25 Machi 2024 hadi tarehe 27 Machi 2024.
TAFADHALI ZINGATIA: Mafunzo ya Taasisi ya Taaluma ya Wanyamapori yanafuata mfumo wa Jeshi Usu (paramilitary). Wote waliochaguliwa wanawajibika kuchukua fomu ya kupimwa afya zao katika Hospitali ya Wilaya, Mkoa au Rufaa. Kutokuzingatia hilo kutakuondolea sifa ya kujiunga katika mafunzo.
BONYEZA HAPA KUPAKUA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA MACHI 2024
BONYEZA HAPA KUPAKUA FOMU YA MAELEZO YA KUJIUNGA NA KOZI YA BTCWLE Na. 60
BONYEZA HAPA KUPAKUA CONTROL NUMBER ZA KULIPIA ADA
BONYEZA HAPA KUPATA ORODHA YA VIFAA NA BEI VINAVYOPATIKANA KATIKA DUKA LA TAASISI
Imetolewa na;
Mkuu wa Taasisi
15 Machi 2024