Campus Life
Campus life
demo
demo
deom
demodeoq
Wahifadhi wa Wanyamapori walipwe vyema
Shirika la ulinzi wa wanyama duniani WWF linataka walinzi wa wanyama pori katika mbuga za taifa kwenye mataifa ya Afrika walipwe fedha maalum kwa kuwakamata majangili.
Serikali ya Ujerumani inatoa fedha kwa ajili ya eneo la bonde la mto Kongo na kuwezesha kile kinachoitwa malipo ya kazi kwa walinzi wa mbuga ya wanyama ya Salonga , ambao pia wanapatiwa fedha hizo maalum. Immo Fischer , msemaji wa WWF nchini Ujerumani akijibu swali la DW amesema:
"Fedha za kuwalipa walinzi wa mbuga za wanyama , ni jambo la kawaida na linatumika katika nchi nyingi za Afrika. Walinzi wa mbuga za wanyama wanafanya kazi za hatari sana, na muhimu sana, na kutokana na kazi hizo muhimu matokeo yake ni malipo."
Mtu anapaswa kutambua kuwa , wazo hili limetokana na haja ya kupunguza rushwa. Wakati mlinzi wa mbunga ya wanyama akimkamata jangili na jangili huyo ana pembe mbili kwa mfano za tembo, malipo yake ya mwaka yataongezeka haraka. Kwa malipo haya kwa walinzi wa mbuga za taifa tunataka kuepuka, kuachiliwa huru kwa majangili kwa kuwapa rushwa walinzi.
Mhariri: Grace Patricia Kabogo