Idara ya Wanyamapori Yaendesha Mafunzo ya Uhifadhi na Usimamizi wa Ardhioevu Tanzania

Idara ya Wanyamapori Yaendesha Mafunzo ya Uhifadhi na Usimamizi wa Ardhioevu Tanzania
Mafunzo yakiendelea kwa Vitendo katika eneo la eneo la uwanja wa ndege wa Mwanza Wakunzi wa mafunzo hayo ni Bw. Lotha Laisser na Imani Nkuwi kutoka Idara ya Wanyamapori, Priscila Mbwaga (TAMISEMI),

Awamu nyingine itafanyika mwaka wa fedha 2012/13 na itawahusisha wasimamizi themananini na wawili (82) wa Ardhioevu katika Wilaya ambazo Programu ya SWM haikutekelezwa.

Mafunzo yakiendelea kwa Vitendo katika eneo la eneo la uwanja wa ndege wa Mwanza Wakunzi wa mafunzo hayo ni Bw. Lotha Laisser na Imani Nkuwi kutoka Idara ya Wanyamapori, Priscila Mbwaga (TAMISEMI), na Simon Mroso, Jane Njau, Charles abachi (Pasiansi) na Nassoro Wawa kutoka Malihai Tanzania.

Idara ya Wanyamapori imekusudia kuingiza mafunzo ya Usimamizi Endelevu wa Raslimali ya Ardhioevu katika mtaala wa Taaluma katika Chuo cha Uhifadhi na Usimamizi wa Wanyamapori cha Pasiansi, Mwanza. Mafunzo haya yametolewa kwa awamu mbili. 

Awamu ya kwanza ilianza tarehe 03/06/2012 na kumalizika tarehe 9/06/2012. Na awamu ya pili ilimalizika tarehe 16/06/12. Awamu zote mbili zinatarajiwa kuwajengea Maafisa mipango, Maji, Mazingira, Uvuvi/Wahifadhi na Wasimamizi wa Ardhioevu themanini na wawili (63) katika makundi mwawili (2) katika ngazi za Halmashauri za Wilaya na Mapori ya Akiba yanayotekeleza Programu ya SWM.

Aidha, mwaka 2012/13 idara inatarjia kuanzisha na kuingiza kwenye mtaala wa chuo cha uhifadhi wa Wanyamapori cha Pasiansi mafunzo kwa Askari Wanyamapori yaani Game scouts (Wetlands Extensionists) ambao watakuwa kwenye ngazi ya chini ya usimamizi wa ardhioevu nchini.

Afisa Mawasiliano, Elimu ya Ardhioevu na Elimu kwa Umma, Wizara ya Maliasili na Utalii, Idara ya Wanyamapori, Kisehemu cha Ardhioevu Bw. Lotha S. Laisser amesema, mafunzo haya yanakusudia kuwajengea uwezo maofisa wanaotekeleza Programu ya Uhifadhi wa Ardhioevu kwenye Wilaya 17 na kuiwezesha Chuo cha Uhifadhi na Usimamizi wa Wanyamapori cha Pasiansi kuingiza kwenye mtaala wake mafunzo haya “Sustainable Wetlands Management Institutionalization”.

Mpango stadi wa mafunzo ulishaandaliwa kwa Idara ya Wanyamapori kupitia Kijisehemu cha Ardhioevu na kujaribiwa kabla ya kuanza kufundisha.  Maandalizi ya Mwanzoni yalijikita katika kuwaanda wakufunzi wane (TOT) wa chuo cha Pasiansi ili waweze kukijengea chuo hicho uwezo wa kuendesha mafunzo hayo chenyewe. Mafunzo hayo yaliendeshwa na wataalamu wa ardhioevu wa Idara ya Wanyamapori Bw. Lotha S. laisser, Imani Nkuwi pamoja na Mtaalamu Mshauri masuala ya Ardhioevu Tanzania Bw. John Balarin.

Katika mafunzo haya, idara inakusudia kuwajengea uwezo maafisa wa wilaya wanaosimamia miradi ya uhifadhi wa Ardhioevu kutumia mingozo ipatayo tisa (09) iliyoandaliwa. Aidha, kitabu cha usimamizi endelevu wa Ardhioevu nchini ndio muongozo mama wa uhifadhi wa ardhioevu nchi ambao mingozo hii imechipukia.

Chuo cha usimamizi na uhifadhi wa Wanyamapori cha Pasiansi inashukuru idara kwa kukusudia kutekeleza sheria ya Wanyamapori ya mwaka 2009 kwa kutambua Ardhioevu kuwa na hadhi sawa na maeneo mengine yaliyotengwa na kuhifadhiwa nchini na kupendekeza kufanya mafunzo na kugharamia mafunzo haya kwa kushirikiana na wafadhili (DANIDA).

recommend to friends
  • Google+
  • PrintFriendly