Habari
TANGAZO LA AWAMU YA TATU WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA TAASISI YA PWTI KWA MWAKA 2023/2024

TANGAZO LA WALIOCHAGULIWA KWA AWAMU YA TATU KUJIUNGA NA MAFUNZO MWAKA 2023/2024
Mkuu wa Taasisi ya Taaluma ya Wanyamapori Pasiansi, Mwanza anapenda kuwajulisha waliochaguliwa kujiunga na mafunzo ya Usimamizi wa Wanyamapori na Himasheria (WLE) na Uongozaji Watalii na Usalama (TGTS) katika ngazi ya Astashahada na Astashahada ya Awali kwa mwaka wa masomo 2023/2024. Waliochaguliwa wanatakiwa kuripoti kati ya tarehe 28 hadi 31 Oktoba 2023 kwa ajili ya usajili na mafunzo ya awali ya kupima utimamu wa mwili na afya, kutokuripoti kwa wakati kutakupotezea nafasi ya kusajiliwa. Aliyechaguliwa anawajibika kufika chuoni kuchukua fomu ya kujiunga na Taasisi (joining instruction) na fomu ya vipimo vya afya au aipakue kwenye tovuti ya Taasisi www.pasiansiwildlife.ac.tz. Kwa waliochaguliwa wanawajibika kulipa ada kuanzia Tsh 1,000,000/- kupitia ‘Control number’ zitakazoandaliwa na kuwekwa kwenye tovuti.
Imetolewa na
Mkuu wa Taasisi,
28 Oktoba 2023
BONYEZA HAPA KUPATA TANGAZO LA AWAMU YA TATU KWA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA MAFUNZO
TCWLE NTA L5 FOMU YA KUJIUNGA NA KOZI YA ASTASHAHADA YA UHIFADHI WANYAMAPORI NA HIMA SHERIA
TCTGS L5 FOMU YA KUJIUNGA NA KOZI YA ASTASHAHADA YA KUONGAZA UTALII NA USALAMA KWA WATALII
BTCTGS L4 FOMU YA KUJIUNGA NA KOZI YA ASTASHAHADA YA AWALI YA KUONGAZA UTALII NA USALAMA KWA WATALII
BONYEZA KUPATA CONTROL NUMBER KWA MALIPO YA ADA KWA WOTE WALIOCHAGULIWA
BONYEZA HAPA KUONA VIFAA NA BEI VINAVYOPATIKANA KATIKA DUKA LA TAASISI 2023