Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Taaluma ya Wanyamapori Pasiansi

Habari
TANGAZO LA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KWA AWAMU YA PILI NA TAASISI YA PWTI KWA MWAKA 2022/2023

Mkuu wa Taasisi ya Taaluma ya Wanyamapori Pasiansi, Mwanza anapenda kuwajulisha wafuatao kuwa wamechaguliwa awamu ya pili kujiunga na kozi ya Astashahada ya Awali ya Usimamizi wa Wanyamapori na Himasheria (BTCWLE), Astashahada ya Usimamizi wa Wanyamapori na Himasheria (TCWLE), Astashahada ya Awali ya Uongozaji Watalii na Usalama (BTCTGTS), Astashahada ya Uongozaji Watalii na Usalama (TCTGTS) kwa mwaka wa masomo 2022/2023. Waliochaguliwa wanatakiwa kuripoti kuanzia tarehe 03 hadi 05 Novemba 2022 kwa mafunzo ya awali ya kupima utimamu wa mwili na afya. Aliyechaguliwa anawajibika kufika chuoni kuchukua fomu ya kujiunga na chuo (joining instruction) na fomu ya vipimo vya afya au aipakue kwenye tovuti ya Taasisi www.pasiansiwildlife.ac.tz. Kila aliyechaguliwa atawajibika kulipa kuanzia Tsh 1,000,000 kupitia ‘Control number’ zitakazoandaliwa na kuwekwa kwenye tovuti.

BONYEZA HAPA KUPAKUA TANGAZO LA WALIOCHAGULIWA KWA AWAMU YA PILI NA MAELEKEZO MUHIMU