Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Taaluma ya Wanyamapori Pasiansi

Habari
TANGAZO LA KUITWA KWENYE MAFUNZO ELEKEZI KWA WALINZI WA KAMPUNI YA ULINZI YA PASIANSI (PASCO)

TANGAZO LA KUITWA KWENYE MAFUNZO ELEKEZI

Mkurugenzi wa Kampuni ya Ulinzi Pasiansi Wildlife Security Company Limited (PASCO) anapenda kuwataarifu waombaji kazi wote walioomba kazi ya ulinzi zilizotangazwa na Kampuni na kufanya usaili kuwa wanatakiwa kuripoti katika Taasisi ya Taaluma ya Wanyamapori Pasiansi-Mwanza kwa ajili ya kuanza mafunzo elekezi [orientation & induction] yanayotarajia kufanyika kuanzia tarehe 10/10/2022 hadi.28/10/2022. Washiriki wote wanatakiwa kuripoti tarehe tajwa hapo juu kuanzia saa 2:00 kamili asubuhi kwa ajili ya kuanza mafunzo. Mshiriki atakayeshindwa kufika kwa wakati uliopangwa atakuwa amepoteza nafasi yake.

BONYEZA HAPA KUPAKUA TANGAZO LENYE MAJINA YA WALIOITWA NA MAELEKEZO MENGINE MUHIMU

Imetolewa na:

Mkurugenzi, 

KAMPUNI YA ULINZI-PASIANSI WILDLIFE SECURITY COMPANY LIMITED (PASCO)