• +255 (0)28 256 0333
Pasiansi Wildlife Training Institute (PWTI)
Year Descriptions View / Download
Aug, 2016 TANGAZO LA KUJIUNGA NA MASOMO MWAKA 2016/2017
Mkuu wa Taasisi ya Taaluma ya Wanyamapori Pasiansi, Mwanza anapenda kuwajulisha wafuatao kuwa wamechaguliwa kujiunga na kozi ya Astashahada ya Awali ya Usimamizi wa Wanyamapori na Hima Sheria (BTCWLE) na Astashahada ya Usimamizi wa Wanyamapori na Hima Sheria (TCWLE) kwa mwaka wa masomo 2016/2017. Kwa waliochaguliwa wanatakiwa kuripoti kwa mafunzo tarehe 22 Agosti 2016. TAFADHALI ZINGATIA: Kwa wote waliochaguliwa kwa ufadhili binafsi ili kuthibitisha udahili na nafasi yako wanatakiwa kulipa shilingi 200,000/- ikiwa ni sehemu ya ada ifikapo tarehe 15 Agosti 2016. Kushindwa kufanya hivyo kutapelekea kupoteza nafasi hiyo. Jina la muweka fedha katika fomu ya kuweka fedha benki liwe ni jina la aliyechaguliwa kujiunga na Taasisi na nakala ya fomu ya kuweka fedha benki itumwe kwa Mkuu wa Taasisi, Taasisi ya Taaluma ya Wanyamapori Pasiansi, S.L.P 1432, Mwanza, Nukushi: +255-(0)282560333, Barua pepe: admission@pasiansiwildlife.ac.tz. Akaunti ya benki ya Taasisi ni Jina la Akaunti: Principal, Wildlife Training Institute, Namba ya Akaunti: 31101100029, Benki: NMB.
TANGAZO_LA_KUJIUNGA_NA_PWTI_2016_2017